Header

“Watu wengi wa Instagram ni waswahili”-; Lulu Diva

Msanii  Lulu Diva ambae kwasasa anafanya vizuri na ngoma yake ya ‘Amezoea’ amesema kuwa kinachopelekea Wasanii wengi kutukanwa na kutolewa lugha mbaya kutoka kwa baadhi ya Mashabiki wao hususani Instagram ni kutokana na watu wengi wanaotumia Mtandao huo  kuwa ni ‘Waswahili’.

Akizungumza na Dizzim Online Lulu Diva amesema watu wengi wanaotumia Instagram sio wakweli na wanaigiza sana Maisha ikiwemo kujifanya wanawajua kiundani Mastaa hao kitendo ambacho yeye anaona Watu hao kama  ni Waswahili.

“Watu wengi wa Instagram ni waswahili tusiongee uongo hata mimi mwenyewe ni mswahili nimekubali  na nimetokea uswahili so watu wajuwe kwamba asilimia kubwa ya watu wa Instgram ni waswahili” Amesema Mrembo huyo.

Aidha msanii huyo amewataka watu waache kuamini kila wanachokiona na kukisikia kwa baadhi ya Watu kwenye Mitandao ya kijamii kwani mara nyingi hujiamuria tu kuzungumza Jambo ambalo si sahihi.

Comments

comments

You may also like ...