Header

Wastara afunguka kuhusu kuingia kwenye Muziki

Msanii wa Bongo Movie Wastara Juma amezungumzia kuhusu yeye kufanya muziki kwa mara nyingine tena baada ya kuachia wimbo wa ‘Mama na Mwana’.

Akizungumza na Dizzim Online Msanii huyo ambae kwasasa amekuwa balozi wa Africa kupitia shirika la ‘Asov’ lililopo Nchini Sweden amesema muziki ataendelea kufanya kwasababu ni kipaji chake kingine.

“Mimi nitaendelea kufanya muziki kwasababu sijaanza jana wala juzi ni tangu mwaka 2009 yani tangu kina fulani na fulani hawajatoka mimi nilikuwa nafanya muziki so nitaendela kufanya muziki” Amesema Wastara.

Shirika la ASOV ni shirika lililoundwa na waafrika waishio nchini Sweden kwa madhumuni ya kusaidia Watoto waishio katika mazingira magumu.

Comments

comments

You may also like ...