Header

Hivi ndivyo Billnass atakavyotumia Elimu yake.

Msanii wa Muziki wa Rap nchini Tanzania Billnass ameizungumzia jinsi gani ataitumia Elimu yake ambayo amekuwa akiipambania kwa muda mrefu.

Akipiga Story na Dizzim Online msanii huyo ambae kwasasa anafanya vizuri na Wimbo wake wa ‘Tag ubavu’ amesema itamsaidia katika  kumuongezea maarifa na pia Elimu ni kitu kikubwa sana katika maisha yake.

”Nilitumia muda mwingi kusoma kwasababu nilikuwa nahitaji kusoma na kufahamu baadhi ya vitu na maarifa kwasaabu hata kwenye vitu vya Biblia imeandikwa sehemu pekee unaweza kupata maarifa ni kukaa darasani kusoma so nilikuwa nahitaji kupata maarifa” Amesema Billnass.

Pia msanii huyo amesema Elimu yake ataitumia kwa kutoa ajira kwa vijana wenzie pindi atakapoanzisha Miradi mbalimbali.

Comments

comments

You may also like ...