Header

Maleek Berry aachia kazi mpya yenye jina kama aliyoshirikishwa Harmonize

Mwimbaji na mtayarishaji wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Nigeria na Staa wa ngoma ‘Pon My Mind’ Maleek Shoyebi a.k.a Maleek Berry  ameachia video ya wimbo wake mpya kwa jina ‘Sisi Maria’ kutoka kwenye Album yake ya ‘First Daze Of Winter’ iliyotoka rasmi mwaka huu.

Jina la ngoma hiyo moja kwa moja limeingia kwenye akili za wengi ambao hawakuwahi kusikia wimbo huo na kutamani kusikia Maleek Berry ameimba nini kwakuwa jina linafanana kabisa na hit song ya msanii OmoAkin aliyowashirikisha Skales na Koker ambayo baadae Remix ya wimbo huo ilimshirikisha Staa wa Bongo Fleva, Harmonize.

Video imepokea maoni mengi mazuri kwa jinsi ilivyog’aa kwa rangi ya vitu mbalimbali vya kisanaa vilivyotumika chini ya uongozaji wa UNLIMITED L.A.

Comments

comments

You may also like ...