Header

Adabu Steven awajibu wanao lalamikia jina la wimbo wake wa ‘IFUNANYA’

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo mwenye makazi yake Texas, Marekani ameamua kuzungumzia sababu za kuona hakuna tatizo katika kuchagua jina la wimbo na wimbo wake kufanana na jina la wimbo uliowahi kufanya vizuri wa zamani wa kundi la zamani la muziki kutoka nchini Nigeria P-Square ‘Ifunanya’.

Akipiga Stori na Dizzim Online, Adabu amesema kuwa kwake ni jambo la kawaida sana majina kufanana na wimbo wake huo kufanana na wimbo wa P Square sio tatizo kwakuwa mashabiki wanapata Burudani ya alichoimba na sio undani wa jina. Adabu ameongeza kuwa kwanza wazo la wimbo kuitwa ‘Ifunanya’ mizuka ilianzia studio na mwisho akajikuta jina la Ifunanya linabaki kuwa jina la wimbo.

“i remember that time when i was recording this…sikuwa na wazo kuwa baadhi watajiuliza kuhusu jina, i did my artisitc job na Good thing ni kwamba song has gone too far and fast na mpaka nyumbani DRC inafanya poa sana tena sana. So! for me i sioni tatizo kuhusu jina la wimbo kufanana na lao P Square, and you know song nyingi ufanana but kinacho-matter ni creativity na vibe of a particular song Basi!.” Amesema Adabu.

Hata hivyo Adabu ameongeza kuwa, zipo kazi nyingi nzuri zimeisharekodiwa na muda wowote ataanza kupakua moja baada ya nyingine na mashabiki wasishangae kuona kuna baadhi ya nyimbo zitafanana majina na nyimbo za wasanii wao pendwa lakini na zikawa ni nyimbo kali kuliko nyimbo za wasanii wao.

“ninachowahadi mashabiki ni kupata kazi muzuri kutoka kwangu na wasishangae kukutana na some of my songs having a similar title na nyimbo ya msanii unayempenda lakini ngoma yangu ikawa kali kushinda yake” Aliongeza.

 

Comments

comments

You may also like ...