Header

Wema Sepetu achafua mtandao kwa Ua Jekundu

Mrembo na Staa wa Bongo Movie, Wema Sepetu amegeuka topic inayohusu mapenzi mara tu baada ya kupost picha ya UA Rose(Ua jekundu) na kuweka maelezo kuwa kwake ni ishara ya upendo na waliowengi kuwanza kuhusisha haina hiyo ya post na ile ya UA Jeusi alilopost Zari The Boss siku ya wapendanao na kuweka maelezo ya kuachana kimapenzi na Diamond Platnumz.

 

Muda mfupi baadae Post hiyo ya Wema Sepetu ilirepostiwa na DJ rasmi wa Diamond Platnumz, Romy Jones na kuacha maneno kwa baadhi ya watu walioanza kuona kama kuna kitu nyuma ya Staa huyo wa Bongo Movie ambacho baadhi wanakijua na kitaanza kujitokeza katika njia tofauti inayowaacha watu wakijuliza maswali.

Katika uwanja wa maoni wa Post hiyo ya Romy, Wema Sepetu aliingia na kuandika kitu chenye chembe za kumpa mtu mmoja uthamani na upekee katika maisha ya watu wake wanaoweza kufika milioni(One In a Milioni).

“My 1 in A million…All Day errday” Aliaandika.

Hili la mazungumzo ya kimtandao kati ya Rj The Dj ‘Romy Jons’ na Mrembo Wema Sepetu ni muendelezo wa tukio la kabla la kimtandao la Romy alipoweka picha ya Wema Sepetu kwenye ukurasa wake wa Instagram katika kutoa taarifa yak kuwa wimbo mpya wa Diamond Platnumz aliomshirikisha Staa wa Marekani, Omarion ‘African Beauty’.
“@Harmonize: One Peace in Town #AfricanBeauty.

Upande mwingine tena maswali yaliibuka juu ya kumuhusisha Wema Sepetu na Diamond Platnumz baada ya Harmonize kumtaja Wema Sepetu katika Post ya Diamond Platnumz kipande cha Video cha wimbo wake wa African Beauty na kuwataka watu matag African Beauty wanayemjua.

Kinachoaminika kutoka katika kinywa cha Wema Sepetu juu ya ukaribu wake na WCB Wasafi hasa katika ujio wa kituo cha Wasafi Tv na Wasafi Radio ni kuwa Wema atakuwa na kipindi katika kituo hicho na bado a;lithibitisha kuwa yeye na Diamond Platnumz ni washikaji na wamefikia hatua ya kuwa Boss na mfanya kazi.

Je’ Unadhani ni nini kinaendelea katika haya yanayoonekana kwa nje kuhusu Wema na WCB Wasafi.

Nini maoni yako??

Comments

comments

You may also like ...