Header

Timmy T Dat azibua mpya na ya kwanza akiwa pekee yake

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Kenya na Staa ngoma ya ‘Wele Wele’ Timothy Owuor a.k.a Timmy T Dat ameachia wimbo wake mpya kwa jina ‘Kitambo’ chini ya utayarishaji wa Prodyuza Musyoka.

Baada ya Timmy kufanya vizuri katika kolabo ya kuwakilisha mitaa wanayotokea na Rapa Khaligraph Jones kwa jina ‘Kasayole’ ngoma yake hii mpya imetoka sambamba na video iliyoongozwa na Director Enos Olik chini ya kivuli cha kampuni yake ya EOP Films.

Wimbo huu wa pekee yake kwa mwaka wa 2018 wenye maadhi ya Danso Timmy umezungumzia mambo mengi yaliyozingatia sanaa kama msani ikiwa ni pamoja na changamoto za maisha yake ya kutoka chini mpaka alipofikia.

Itazame Video ya wimbo wake huo mpya.

Comments

comments

You may also like ...