Header

Singida United yakanusha kufungiwa kwa Daniel Lyanga(+Audio)

Uongozi wa Klabu ya Singida United umekanusha Taarifa za kufungiwa na FIFA  kwa Mshambuliaji wao Danny Ruben Lyanga ambaye alisajiliwa katika Dirisha Dogo la Usajili Mwaka Jana.

Baada ya kutoonekana ndani ya Kikosi cha Singida kumekua na taarifa kuwa Lyanga amefungiwa na FIFA kwa kile kinachodaiwa kuwa na Mkataba na Singida pamoja na Klabu yake ya zamani ya Fanja FC.

Mkurugenzi wa Klabu ya Singida Festo Sanga amefafanua juu ya Tuhuma hizo na kueleza kuwa Mchezaji huyo hajafungiwa ila kulikua na Matatizo ya ITC kutokana na usajili wake kukamilika wakati Dirisha la Usajili VPL kuwa tayari Limefungwa.

Kwa sasa Klabu hiyo inayoshika nafasi ya nne katika Msimamo wa Ligi inajiandaa na Mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya Robo Fainali dhidi ya Mabingwa Klabu ya Soka ya Yanga Mchezo utakaopigwa April 1 kwenye Dimba la Namfua.

Comments

comments

You may also like ...