Header

Weasal Manizo awasilisha heshima zake kwa Mowzey Radio

Msanii wa muziki kutoka nchini Uganda, Douglas Mayanja a.k.a Weasal Manizo aliyeunda kundi la pamoja na marehemu Mowzey Radio ‘Goodlyfe’ ameachia video ya wimbo wake kwa jina ‘Tokyayitaba’ wimbo wa maudhui ya heshima zake kwa Mowzey Radio.

Wimbo umegusa hisia za wengi kwa kile ambacho awali kilionekana kwenye picha aliwahi kuipost Weasal katika ukurasa wake wa Instagram akiwa amekalia kiti na pembeni yake kukiwa na kiti na kiti hicho cha pili kikiwa kimebandikwa picha ya Mowzey Radio kama uwakilishi wake wa kundi lao la GoodLyfe.

Kazi hii mpya ya Weasal anayefanya kazi chini ya lebo ya muziki ya Goodlyfe Magic imeletwa kwako chini ya Goodlyfe ikishirikiana na Angel Music huku video ikiwa ni chini ya uongozaji wa Director Darlington.

Comments

comments

You may also like ...