Header

Beka Flavour akunjua jamvi la upendo, Amuweka wazi mpenzi wake(+Picha)

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Tanzania, Bakari Katuti a.k.a Beka Flavour ametoa sababu za kumuweka wazi mpenzi wake wa siku nyingi kwa jina Happness Tarimo a.k.a Happie Reuter.

Akizungumza na Dizzim Online, Beka amesema kuwa ni maamuzi na ameona ni vyema kuweka wazi na kuzungumza juu ya mahusiano yake kwakuwa amegundua ni muda muafaka kwa wote wanaopenda kujua hali yake ya kimahusiano.

Happness Tarimo a.k.a Happie Reuter

“Naona sasa hivi watu wajue tu kwasababu hilo swali nimekuwa nikikutana nalo sana, na wenye uchu wa kujua sasa wajue kuwa ni Happy. Na nimeonea niliweke hilo wazi japo nipunguze usumbufu wa akina dada maana nimepata sana shida kipindi chote nilichokuwa sijaweka wazi” Amesema Beka Flovour.

Happness Tarimo a.k.a Happie Reuter

Beka Flavour na Happness Tarimo a.k.a Happie Reuter katika pozi la pamoja

Hata hivyo  Beka bado anafanya vizuri kwa kolabo kama vile ‘Najiona mbali aliyomshirikishwa Bongela Nyau,  Asali’ yake ya Chemical na ngoma zake binafsi ambazo ni Kibenten, Safarina na nyingine nyingi.

Comments

comments

You may also like ...