Header

Khaligraph Jones na Sauti Sol wajiweka tayari kuachia kolabo yao

Kolabo ya Rapa Khaligraph Jones na Kundi la Muziki la Sauti Sol kutoka nchini Kenya imetangazwa kutoka rasmi siku ya Jumatatu na video ya wimbo huo kutoka Jumanne ya wiki ijayo.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Khaligrap amethibitisha hilo na kuwataka wadau na mashabiki wa muziki kupokea kolabo hiyo itakayokwenda kwa jina ‘Rewind’ kupitia njia mpya ya ununuaji muziki kwa kupitia mtandao ya Songa inayomilikiwa na kampuni yasimu ya nchini humo.

“It’s Official, on Tuesday we are finally dropping the Banger but the question is, Are You ready?

Audio out on Monday exclusively on @Songamusic.

#Rewind #SautiSolPapaJones #Rewind#SautiSolPapaJones cc @sautisol” Ameandika katika picha ilioonekana kama itawakilisha Wimbo huo kama Kava.

Comments

comments

You may also like ...