Header

Mzungu apagawishwa na muonekano wa kike wa Janjaro.

Mtayarishaji wa video za muziki nchini Tanzania Nisher amezungumzia changamoto waliyo kutananayo wakati wanatayarisha video ya Dogo janja ‘Wayuwayu’ ambayo imekuwa ikizungumziwa sana katika mitandao ya kijamii kutokana na Dogo janja alivyouvaa uhusikia wa kike.

Akipiga story na Dizzim Online Nisher ambae kwasasa makazi yake ni jijini Dar es salaam amesema kuwa changamoto kubwa waliyokutana nayo ni Dogo janja kuombwa namba ya simu na Mzungu ambae alidhani Janjaro ni mwanamke kutokana na jinsi alivyovaa kama anavyoonekana kwenye Video.

“Wakati tupo tunajianda kushoot Janja alikuwa anaendelea kujipamba pamba sasa kwa upande mwengine kulikua na mzungu alikuwa akimuangalia Janjaro na baadae akamtuma muhudumu wa pale hotelini akamchukulie namba ya Dogo Janja yule muhudumu akamwambia yule ni mwanaume pale kuna kazi wanafanya so ndo changamoto tuliyo kutananayo location” Amesema Nisher.

Aidha Nisher amewaambia mashabiki wa muziki Tanzania ubunifu uliofanyika kwenye video hiyo ya Janjaro utaendelea  kwa wasanii wengine kwani anaamini ni ubunifu wa kipekee sana ingawa kwa nchi zingine ulishafanyika.

Comments

comments

You may also like ...