Header

Babbi Music ateleza mpaka Tanzania, Aangukia kwenye mikono ya Touch Sound

Msanii wa muziki wa kizazi kipya kutoka Burundi mwenye makazi yake mjini Phoenix jimbo la Arizona nchini Marekani, Babbi Music ameachia wimbo wake mpya kwa jina ‘Mbwira’ aliotayarishwa chini ya Studio za Touch Sound.

Wimbo huo unasikika katika uandishi wa lugha ya Kirundi ambayo kwa maana rasmi ya neno ‘Mbwira’ tafsiri yake ni ‘Niambie’ huku utayarishwaji wa Prodyuza Davy Ma-Cord akishirikianana Mr. T Touch kutoka Tanzania ambapo video ya wimbo huyo itatoka hivi karibuni kwa mujibu ya Poster ya msanii huyo kupitia ukurasa wake wa Instagram.

Babbi Music tayari ameshafanya vizuri kupitia nyimbo zake kama vile, Kikomando, Anga La Mpenzi, Till I Die, Sexy Girl na nyingine anaendelea kufanya nyimbo zake chini ya kuvuli cha Babbi Music ambayo iko katika mipango ya kuwa lebo yake rasmi.

Usikilize wimboo huo.

Comments

comments

You may also like ...