Header

DNA apata msiba wa mwanae wa kiume

Staa wa muziki kutoka nchini Kenya, Dennis Kaggia ‘DNA’ amempoteza mtoto wake wa kiume ‘Jamal Waweru’ kwa ajali ya maji.

Mtoto huyo wa Darasa la Tatu katika shule ya Kitengela International, mwenye umri wa miaka 9 amefariki kwa kuzama katika Bwawa la kuogelea(Swimming Pool) siku ya jumatano Mchana akiwa shuleni.

Jamal alifariki katika Hospitali ya Wanawake ya Nairobi iliyoko Lang’ata ambapo mtoto huyo  aliwahishwa kwa Matibabu na baadae Mwili wake ulipelekwa kuhifadhiwa ‘Shalom Funeral Home’.

Comments

comments

You may also like ...