Header

‘Samata A’ azipa thamani kolabo za kulipia, Atoa Sababu za kibiashara

Msanii wa muziki kutoka Tanzania na Staa wa ngoma ya ‘Unanisololo’ aliyomshirikisha Dayna Nyange, Samata A, amejibu juu ya madai ya msanii kulipia kolabo kuwa ni kutoamini uwezo wao binafsi.

Akizungumza na Dizzim Online, Samata ameeleza kuwa Muziki ni biashara ambayo inategemea mitaji mbali mbali katika msingi mkuu wa kipaji na Pesa hivyo inapofika hatua msanii kulipia kolabo inaweza kuwa na maana ya kuthamini ukubwa wa msanii husika na kuleta maana halisi ya muziki ni biashara.

“Jamani watu naamini washajua kuwa muziki ni biashara, sasa ukisema ni kutojiamini mbona mastaa hata wakubwa Duniani wanafanya kolabo na sisi hatujui kama wamelipana lakini ninachojua ni wanashirikiana kibishara na nadhani Duniani kote iko hivyo katika muziki wasanii akiwa na nia ya kibiashara” Alisema Samata A.

“Unaweza kulipa na ukabaki mbovu tu kama hakuna kipaji na hujafanya kwa lengo ka kukuza biashara ya muziki wako. Mfano mimi Nina ngoma nilizoachia na sio kolabo lakini watu wanaweza kuwa wanazijua na kuzipenda zaidi ya nilizoshirikiana na mtu tena mkubwa kwenye Game” Aliongeza.

Samata A anafanya vizuri na ngoma yake mpya inayokwenda kwa jina ‘Aah Kodo’ ambayo iko katika mipango ya kuandaliwa video na muda wowote video ya wimbo huo ikiwa tayari ataiachia rasmi.

Hii ni kolabo ya wimbo wake aliomshirikisha Staa wa kike wa Bongo Fleva, Dayna Nyange.

Comments

comments

You may also like ...