Header

TID atangaza kufunga ndoa nchini Ujerumani

 

Mkongwe wa muziki wa Bongo Fleva, Khalid Mohamed ‘TID’ amezungumzia kufunga ndoa na mpenzi wake na anabainisha kuwa ndoa yake hiyo itafungwa mjini Munich nchini Ujerumani.

TID ametangaza kuwa yuko ndani ya dimbwi zito la upendo na mrembo ambaye kwa haraka jina lake halijatambulika ambaye kwa mara kadha wamekuwa akitokea katika picha ya pamoja ambapo mara hii ameweka picha yake akiwa amelalaiwa kifuani na mrembo huo na kuandika ujumbe ufuatao:-

@tidmusic: “Happy Easter Guys…Only Sky is a Limit,Never Let anyone Put you Down this Holiday,from the bottom of my Heart I Shud make it Clear to everyone Else,Am in LoVe”.

Kwenye post ya Picha hiyo alijitokeza mtu wa karibu wa TID kwa utambulisho wa akaunti yake ay Mtandao wa Instagram kwa jina ‘ucngiz’ aliyeandika “Top of the Top Mnyama” ambapo katika kujibiwa, TID aliandika “@ucngiz: Dah Mkali wangu u need to provide me with your travel documents zako wewe na Fread so that u can be able to attend my Wedding in July here in Munich”.

Bila shaka mapenzi ni moto moto na wapenzi hao washafikia hatua ya kuamua kuishi kama mke na mume ambapo TID kwa sasa yuko nchini Ujerumani na mpenzi wake huyo.

Comments

comments

You may also like ...