Header

Steven Nyerere aitupia lawama kamati ya maandalizi Tuzo za ‘Sinema Zetu’

Muigizaji na Mchekeshaji kutoka Bongo Movie Steven Nyerere, Ameikosoa kamati ya Tuzo za ‘sinema zetu’ ambazo ziliandaliwa na Azam Tv na kufanyika  Mlimani City Jijini  Dar es salaam siku ya tarehe 1 April.

Akizungumza na Dizzim Online Steve ambae alipata umaarufu kwa kuuvaa uhusika wa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere amesema kamati haikujipanga vizuri kwenye kuandaa vipengele vya kugombania Tuzo hizo.

“Kamati imejichanganya sana kwenye vile vipengele  vya Tuzo huwezi kumuweka Wema Sepetu na ukamuacha Liyama Ally au ukaacha kumuweka Johari au Wolper na wengine wengi tunaowaona wanafanya vizuri sina maana kwamba Wema hakustahili hapana ila wangewaweka na wengine kwenye hiko kipengele au unamuweka Gabo alafu unamuacha Ray au Mzee Majuto  kina Jb kina Single Mtambalike hii sio sawa”  Amesema Steven Nyerere.

Aidha mchekeshaji huyo amewaomba waandaaji wa Tuzo hizo waangalie upya upangaji wa vipengele hivyo ili itakapofika mwakani  isijirudie tena, pia amewapongeza washindi wote wa Tuzo hizo.

Comments

comments

You may also like ...