Header

Nikki Mbishi aishuhudia ‘NIMEKUMISS’ kupitia Wasafi Tv, Atoa Shukrani zake

Msanii wa muziki wa rap kutoka Tanzania, Nicas John Marwa Machuche a.k.a Nikki Mbishi ametoa shukrani zake kuelekea kituo kipya Tanzania cha Wasafi Tv kwa kucheza wimbo wake wa ‘Nimekumiss’.

Moja ya sababu zilizomtia moyo na kushauri utaratibu uliotumika usibadilike na kituo hicho kupata nakala ya wimbo huo bila kupelekewa kwakuwa video ya wimbo huo inapatikana mtandaoni.

“#WASAFITV nyie mmecheza wimbo wangu #NIMEKUMISS bila hata mimi kuwaletea,najua ndio mnaanza ila msisahau kuendelea hivi hivi.

Hakuna kitu kinachojenga na kuimarisha misingi ya sanaa kama ushindani wenye usawa “Fair Competition” hii inamaanisha anayestahili na apate na asiyestahili akose japo #FITNA zipo tu.

Tumeshuhudia umwinyi na ubeberu kwa kipindi kirefu sana,wapo ambao walitaka uMungu mtu lakini walijishtukia wakabwaga na wengine walibwagwa na hiyo ni kwa sababu ya kuleta umatabaka wa kanda fulani na kanda fulani na kujuanajuana sana kiasi kwamba akina sisi tusiofungamana nao tukaishia kutengwa na kuonekana “VINEGA”

Kila la kheri kwenye hii ligi ya mbuzi kuna siku daraja litapanda tutacheza ya ng’ombe na mpaka tembo nini simba.

Ipo siku watajihoji na kujijibu wenyewe.

Cc @wasafitv” Aliandiska kupitia Ukurasa wake wa Instagram ambapo aliweka picha ya Tv hiyo alipokuwa akicheza wimbo huo.

 

Asante #WASAFITV nyie mmecheza wimbo wangu #NIMEKUMISS bila hata mimi kuwaletea,najua ndio mnaanza ila msisahau kuendelea hivi hivi. Hakuna kitu kinachojenga na kuimarisha misingi ya sanaa kama ushindani wenye usawa "Fair Competition" hii inamaanisha anayestahili na apate na asiyestahili akose japo #FITNA zipo tu. Tumeshuhudia umwinyi na ubeberu kwa kipindi kirefu sana,wapo ambao walitaka uMungu mtu lakini walijishtukia wakabwaga na wengine walibwagwa na hiyo ni kwa sababu ya kuleta umatabaka wa kanda fulani na kanda fulani na kujuanajuana sana kiasi kwamba akina sisi tusiofungamana nao tukaishia kutengwa na kuonekana "VINEGA" Kila la kheri kwenye hii ligi ya mbuzi kuna siku daraja litapanda tutacheza ya ng'ombe na mpaka tembo nini simba. Ipo siku watajihoji na kujijibu wenyewe. Cc @wasafitv

A post shared by NIMEKUMISS (@nikkimbishi) on

Comments

comments

You may also like ...