Header

Otile Brown atoa jibu halisi kuhusu Picha ya Harusi yake

Msanii wa muziki kutoka nchini Otile Brown ametoa jibu la picha aliyoonekana anaoa kwa kuachia kolabo ya wimbo wake mpya unaokwenda kwa jina ‘’Chaguo la Moyo’.

Kolabo hiyo imemshirikisha Mwimbaji Snaipei Tande ‘Sanaipei’ na ndiye anayeonekana kuwa Bibi harusi katika video ya wimbo huo ulioongozwa Director X Antonio kutoka nchini Kenya.

Dizzim Online wiki chache zilizopita ilisharipoti juu ya Otile Brown kukutana Studio na Mtayarishaji Teddy B ambapo katika utayarishaji ambapo awali haikuwekwa wazi kuwa wimbo utamshirikisha Snaipei.

Comments

comments

You may also like ...