Header

Hope Kid awakumbusha wasanii wa Injili wanaopotea

Msanii wa muziki wa injili kutoka nchini Kenya, Simon Peter ‘Hope KID’ ameachia video ya wimbo wake Mpya kwa jina ‘HUDUMA’ wenye maudhui na lengo la kuwakumbusha wasanii wa muziki wa injili waliojisahau katika kulitangaza neno na kutumia muda wao mwingi katika biashara na umaarufu.

Wimbo huo unamkumbusha kila msanii aliyeanza hatua za kulitangaza neno kama msanii wa muziki wa Injili kuendelea na utaratibu huo na hiyo imetokana na mtazamo wake kuwa wapo baadhi waliobadili upepo na kuchukua muelekeo tofauti ulio nje ya imani na mafundisho.

Wimbo umetoka chini ya Drama House Music kwa utayarishaji wa Prodyuza Vicky Pon Dis ambapo video imeongozwa na Director Trey Juelz.

Itazame video ya wimbo huu mpya wa Hope Kid.

Comments

comments

You may also like ...