Header

Mr. Eazi na Prezzo kwenye umati wa mashabiki nchini Kenya

Msanii wa muziki kutoka nchini Nigeria Oluwatosin Oluwole Ajibade ‘Mr. Eazi’ anmeweka picha yake kwenye mtandao wa instagram akiwa katika hatua za uchukuaji wa kumbukumbu ya picha na mashabiki wake mjini Nairobi nchini Kenya.

Eazi yuko nchini humo katika ziara ya wimbo wake mpya ‘Happy Boy’, ziara hiyo iliambatana na zoezi la kuwalipia mashabiki 120 wa muziki wake kwenda CINEMA kutazama filamu ya kikenya ambapo katika picha hiyo anaonekana Rapa kutoka nchini humo, CMB Prezzo.

Eazi katika ziara hii pia atatoa burudani ya muziki siku ya kesho katika kumbi wa Walter Front ulioko Ngong Racecourse nchini humo.

Comments

comments

You may also like ...