Header

Pep Guardiola;-“Mino Raiola (Wakala) alinipa Ofa ya kumsajili Pogba Januari”

Kocha wa Manchester City Pep Guardiola amefichua kuwa Wakala maarufu wa Wachezaji Barani Ulaya Mino Raiola alimpa Ofa ya kuwasajili Viungo Paul Pogba pamoja na Henrich Mkhitaryan Mwezi Januari Mwaka huu.

Guardiola amemjibu Wakala wa Pogba baada ya kitendo chake cha kumtolea maneno mabaya kocha huyo kwa kumuita Mbinafsi pamoja na Muoga.

“Naweza kumjibu(Raiola), Nashindwa kuelewa kwanini aseme mimi ni Mtu mbaya, sijawai kuzungumza nae hivyo Maneno yake kuhusu mimi hayana tija. Miezi Miwili iliyopita alinipa Ofa ya kuwasajili Pogba na Mkhitaryan wajiunge na Sisi (Man City). sasa kwanini aniite Mbaya na awe tayari kunipa Wachezaji wake?. Alisema Guardiola.

Baada ya maneno hayo Mino alijibu pia kuwa hajawai na asingeweza kuzungumza na Guardiola kuhusu dili hilo ila anaweza kuzungumza na Klabu ya Man City kwa sababu ni Klabu kubwa sana.

Mino Raiola na Guardiola wamekuwa na tofauti tangu kipindi Kocha huyo yupo Barcelona ambapo Mteja wake Zlatan Ibrahimovic alikuwa hapewei nafsi katika kikosi cha Barca mpaka akaamua kuondoka na kujiunga na Ac Millan.

Comments

comments

You may also like ...