Header

Abela Music apata watoto mapacha, Mmoja apewa jina la Izzo Bizness

Msanii kutoka katika kundi la muziki la ‘The Amaizing’, Abela Music amejifungua watoto mapacha na mtoto mmoja kati ya watoto hao wawili amepewa jina halisi la msanii wa muziki anyeunda kundi hilo Izzo Bizness ‘Emmanuel’.

Abela Music

Abela kupitia ukurasa wake wa Instagram siku ya jana alipost picha iliyomuonesha akiwa chumba cha kujifungulia ‘Labour Room’ na kuthibitisha kuwa mwezi Februari 22 mwaka huu wa 2018 alifanikiwa kupata watoto mapacha na wamepewa majina ya  ‘Enala’ na ‘Emmanuel’.

Hata hivyo Izzo na Abela mara zote kila walipoulizwa na vyombo vya habari wamekuwa wakikanusha kuwa namahusiano ya kimapenzi na kuhusu kupata watoto hao mwanakikundi cha The Amaizing, Izzo Bizness hajapost chochote.

Abela Music na Izzo Bizness

Comments

comments

You may also like ...