Header

Darassa awaondoa ‘HOFU’ Mashabiki juu ya kimya chake

Rapa na Staa wa wimbo wa ‘Muziki’ kutoka Tanzania, Shariff Thabeet a.ka Darassa ameiambia Dizzim Online kuwa mashabiki wa muziki wake, wadau wa Burudani na Raia wema waondoe hofu na wasiwe wepesi wa kuamini chochote kibaya juu yake kinachozungumzwa na wasio na ushahidi wake.

Akipiga story na chumba chetu cha habari kwa njia ya simu, Darassa amesema kuwa yeye ni mzima wa Afya na anaendelea majukumu yake ya kila siku ikiwa ni pamoja na kuandaa nyimbo kwa ajili ya mashabiki wa muziki wake na kuitendea haki tasnia ya Burudani ndani na nje ya Tanzania.

“Jamani mimi niko poa kabisa, maneno yanayosemwa na watu sidhani kama yanahitaji kuaminika kama sijasema mimi au pasipo na ushahidi. Niko poa na naendelea na mitikasi yangu, Studio kama kawa na pale nitakapoweka mambo yangu sawa kwa maana ya kuwa tayari kuwafahamisha chochote mashabiki wangu, watajua tu. Ila kwa sasa nimeamua iwe hivyo inavyoonekana” Amesema Darassa.

Darassa amekuwa kimya baada ya kuachia wimbo wake wa ‘Hasara Roho’ ulitoka miezi 11 iliyopita na kupitia ukurasa wake wa Instagram wenye zaidi ya wafuasi laki tano kwa mara ya mwisho aliweka picha yake ya safari ya ndege mwaka jana mwezi wa Nane.

Comments

comments

You may also like ...