Header

Wanafunzi wa Watanzania waingia Tuzo za Kimataifa za DStv Eutelsat Star

 

  • Tanzania kutetea ushindi ilioupata msimu uliopita
  • Ilboru, Al-Madrassat Ussaifiyatul Burhaniyah zaongoza

Jumatatu Aprili 9, 2018; Tanzania imepata wawakilishi wawili watakaoshiriki katika msimu wa saba wa tuzo maarufu barani Afrika kwa wanafunzi wapenzi wa masomo ya Sayansi na Teknolojia ijulikanayo kama – DStv Eutelsat Star Awards. Wanafunzi hao Michael Ditrick wa shule ya Sekonday Ilboru – Arusha na Taher Rasheed wa Al-Madrasat Ussaifiyatul Burhaniyah ya jijini Dar es Salaam

Michael ameshika nafasi ya kwanza katika uandishi wa insha maalum na Taher kwa mchoro maalum kuhusiana na sayansi ya Setelait ambapo wanafunzi zaidi ya 150 kutoka shule mbalimbali nchini walishiriki katika mashindano hayo ya mwaka huu. Washindi hao walipatikana kutakana na utahini uliofanywa na jopo la majaji sita.

Kazi za washindi hao zimewasilishwa MultiChoice Africa ambapo zitapambanishwa na kazi kama hizo kutoka kwa washindi wa nchi nyingine kote barani Afrika na hatimaye kupatikana mshindi wa jumla katika kila kipengele yaani wale walioandika insha na wale walioandaa mchoro.

Mkurugenzi Mtendaji wa MultiChoice Tanzania Maharage Chande, amesema tuzo za mwaka huu zimekuwa na ushindani mkubwa ambapo shule kutoka mikoa mbalimbali ikiwemo Mwanza, Dar es Salaam, Mbeya, Arusha, Dodoma, Pwani zimeshiriki. “Kuongezeka wa idadi ya wanafunzi wanaoshiriki katika tuzo hizi ni ishara njema na tunaamini kwa viwango walivyoonyesha, bila shaka mwaka huu tutapata ushindi mkubwa kuliko hata ule wa mwaka jana” alisema Maharage.

Amesema tuzo hizi zinalenga kuwajengea vijana wetu ari ya kushiriki katika masomo ya sayansi na pia kuhamasisha ubunifu na ugunduzi katika tasnia ya sayansi. Amewataka walimu kuwahimiza wanafunzi wao kushiriki katika tuzo kama hizi za kimataifa kwani ni kipimo kizuri kwa wanafunzi wetu na pia inajenga kujiamini kwa wanafunzi wetu.

Tuzo hizi ambazo zinahusisha uandishi wa insha maalum au kuandaa bango vyenye ujumbe kuhusiana na elimu ya anga hususan Setelait ni za wazi kwa wanafunzi wote wa shule za sekondari wenye umri kati ya miaka 14 – 19.

Mwaka huu, washindani walitakiwa kuandika insha au kubuni bango kuhusu manufaa yaliyoletwa na uvumbuzi wa setelaiti katika maisha ya kila siku hapa ulimwenguni na ni jinsi gani setelait imekuwa kama kiungo muhimu kwa shughuli zote zinazofanyika kote duniani.

Kama kawaida tuzo hizi zina zawadi kabambe ambapo mshindi wa Insha atapata fursa ya kuzuru kituo cha Eutelsat nchini Ufaransa na pia kwenda Guiana kushuhudia mubashara urushwaji wa setelait angani.

Mshindi wa bango atajishindia safari ya kwenda nchini Afrika Kusini na kutembelea kituo cha anga cha nchi hiyo na pia makao makuu ya MultiChoice Africa akiwa kama mgeni maalum.  Shule zitakazotoa washindi hao zitapata zawadi ya kufungia huduma ya DStv bure.

Wanafunzi wengine waliofanya vizuri katika mchakato huo ni pamoja na Pio Mwita wa UWATA Sekondari ya Mbeya ambaye ameshika nafasi ya pili kwenye insha na Peter Kiama wa Feza Boys ya Dar es Salaam aliyeshika nafasi ya pili kwa upande wa bango.

Mwaka jana Tanzania iliibuka mshindi wa pili kwenye insha baada ya Davids Bwana wa FEZA Boys kunyakua nafasi hiyo nyuma ya mwanafunzi Leoul Mesfin kutoka Ethiopia.

 

About Eutelsat                                                    

Founded in 1977, Eutelsat Communications is one of the world’s leading satellite operators. With a global fleet of satellites and associated ground infrastructure, Eutelsat enables clients across Video, Data, Government, Fixed and Mobile Broadband markets to communicate effectively to their customers, irrespective of their location. Over 6,700 television channels operated by leading media groups are broadcast by Eutelsat to one billion viewers equipped for DTH reception or connected to terrestrial networks. Headquartered in Paris, with offices and teleports around the globe, Eutelsat assembles 1,000 men and women from 32 countries who are dedicated to delivering the highest quality of service.

For more about Eutelsat go to www.eutelsat.com

About MultiChoice Africa

Entertainment is a powerful way to tell stories that open our minds, bring people together around shared passions, and connect us to new realities. It makes us laugh and cry. It informs, it educates and it inspires. MultiChoice is a video entertainment company, and our purpose is to enrich lives. We make the best in entertainment accessible to millions of households in 49 countries across Sub-Saharan Africa. We do this through cutting-edge technology on our DStv and GOtv platforms – delivering the content our customers love and contributing to the success of local economies. Born and bred in Africa, we are rooted in the countries where our customers live. We are managed and run by local people, and strive to provide all our employees with new opportunities. We’re proud of the contribution we make to our communities, and our business has grown hand-in-hand with local economies by forging long-term partnerships with governments, national broadcasters and entrepreneurs. We want to use our influence and resources to play a positive role in Africa, helping to grow Africa’s people and creative industries into vibrant, economic powerhouses. It’s by creating value for our customers, our employees and society that we’ll build a successful business for the future.

Comments

comments

You may also like ...