Header

Willy Paul na Harmonize waja na Pilipili

Moja ya kazi za muziki zilizodaiwa kuwa zitakuwa kubwa kutoka kwa msanii wa nchini Kenya na mmiliki wa lebo ya ‘Saldido Records’, Wilson Shikwekwe Radido a.k.a Willy Paul ni kolabo hii aliyomshirikisha Staa wa Bongo Fleva kutoka lebo ya WCB Wasafi, Harmonize inayokwenda kwa jina ‘Pilipili’.

Wimbo huu unakwenda kwa jina ‘Pilipili Remix’ ambao toleo lake la awali la audio lilitoka rasmi mwezi wa Sita mwaka jana chini ya utayarishaji wa Prodyuza Teddy B katika Studio za Saldido Records na Remix hii inatoka sambamba na video iliyoongozwa na True D Pictures.

Comments

comments

You may also like ...