Header

Wahu aweka nyingine juu ya Uokovu wake baada ya ‘SIFA’

Msanii wa mziki kutoka nchini Kenya na mke wa Msanii David Mathenge a.k.a Nameless, Wahu Kagwi ‘Wahu’ baada ya kutangaza kuokoka rasmi mwaka jana, ameachia video ya wimbo wake mpya wa Injili baada ya wimbo wa ‘SIFA’ uliotoka mwaka jana.

Wahu Kagwi

Wazo kuu la wimbo huu unaokwenda kwa jina ‘My Everything’ limetengenezwa na Muimbaji wa Injili wa nchini humo, Pitson chini ya Pitson Pen & Paper na uandishi kukamilishwa kwa ushirikiano na Wahu Kagwi ambapo audio imetayarishwa na na Prodyuza Teddy B na video imeongozwa chini ya True D Productions.

Katia mahojiano yake tofauti na vituo vya matangazo nchini Kenya, Wahu amekuwa akiweka wazi kuwa hatua ya kuokoka kwake ni maamuzi ambayo hayaegemei katika kipaji cha yeye kufanya muziki bali limekuwa ni tamanio la moyo wake kufanya maamuzi hayo yaliyokamilisha mwezi Novemba, mwaka 2016.

Itazame Video ya wimbo huo mpya.

Comments

comments

You may also like ...