Header

BAHATI AMTAMBULISHA MSANII MPYA KUPITIA LEBO YAKE YA EMB!

Bahati Kushoto Akiwa Na Rebecca Soki Msanii Mpya Kwenye Lebel EMB

Msanii wa nyimbo za injili kutoka Kenya Kevin Bahati a.k.a Bahati Tena, jana usiku katika ukumbi wa KICC jijini Nairobi Kenya aliweza kumtambulisha msanii wake wa tatu chini ya uongozi wa record lebel yake ya EMB (Eastlands Most Beloved). Tayari record lebel hiyo iko na wasanii watatu wakiwemo Mr. Seed na David Wonder. Sherehe ya kuzinduliwa kwa msanii huyo mpya, ilianza mapema jana usiku mda wa saa mbili usiku, huku mashabiki na wadau mbalimbali wa muziki nchini Kenya wakihudhuria kwa wingi. Na kati ya watu mashuhuri walio hudhuria hafla hiyo alikuwemo pia mkurugenzi wa kitengo cha kushughulikia wateja kutoka kampuni ya mawasiliano nchini Kenya ya Safaricom Bi. Slivya Mulinge.

Bi. Slivya Mulinge Akitoa hotuba kwenye uzinduzi huo

Msanii mwenyewe ambye kwasasa ndio amejiunga na lebel EMB  inayomilikiwa na Bahati, anajulikana kama Rebecca Soki. Anaweka idadi ya wasanii wa EMB  kuwa wasanii wanne akiwemo Bahati mwenye. Usiku huohuo pia kibao cha msanii Rebecca Soki chini ya uongozi wa lebel ya EMB kilizinduliwa natayari kinapatina kupitia account ya YouTube kwa jina Baraka zangu. Mfumo wa kufanya kazi chini ya recording lebels kwa wasanii wa Africa, umeaanza kuzaa matunda. Hii ni ishara kuwa sanaa ya muziki inakua kwa kasi na imekuwa kitega uchumi kwa vijana wengi hivyo serikali zetu zinafaa kutilia maanani umuhimu wa sanaa na kuweka miundo msingi bora kwa wasanii ili waweze kuinua uchumi wa nchi husika za kiafrica mfano wanavyo fanya wenzetu kule ughaibuni.

Wasanii wote wa EMB wakiwa kwenye Redcarpet. Kutoka kushoto, David Wonder, Bahati, Rebecca Soki na Mr. Seed

Comments

comments

You may also like ...