Header

MSANII BEKA the BOY AKITA KAMBI NAIROBI KWA AJILI YA UZINDUZI WA KIBAO NYOTA!

Nyota ya msanii Beka the Boy ambaye chimbuko lake ni pwani ya Kenya, inazidi kung’aa hii ni baada ya kupata usimamizi  tabithi chini ya lebel yake ya Double B. Beka ambaye vibao vyake Niko Low, Siri ya moyo, Jidai na vingine vingi vitamu ambavyo viliwavutia mashabiki lukuki na kumfanya kuwa miongoni mwa wasanii wakali wanao wakilisha pwani ya Kenya vyema Africa Mashariki. Safari ya muziki ya nguli huyu imekuwa na changamoto nyingi sana, ila kwasasa inaonekana milango ya neema imefunguka na sasa tayari yuko jijini Nairobi ambako tayari amerekodi muziki na kutengeneza video kwa mtayarishi wa muziki nguli Dr. Eddy wa Dreamland music company na pia mtayarishiji makali wa video Africa Kevin Bosco.

Itakumbukwa kuwa Dr. Eddy ndiye aliyehusika kwa kina katika harakati ya kumuinua na kumtambulisha msanii kutoka Pwani ya Kenya simwingine bali Otile Brown a.k.a Shivoo. Kevin Bosco pia amekuwa katika mstari wa mbele kutengeneza video zenye ubora za mastaa wengi wa Africa mashariki akiwemo Dr. Jose Chameleon, King Kaka, Avril, Ommy Dimpoz na wengine wengi. Tayari chini ya uongozi wa mtayari huyu nguli wa video Kevin Bosco, Beka the Boy ameachia video yake yenye viwango vya kuvutia kwa jina nyota huku akijitayarisha kuachia vibao vingine kwa mpigo akiwa chini ya mikono ya Dr. Eddy na kevin Bosco. Wakati harakati hizi zikiendelea itakumbukwa kuwa Beka the Boy, anajitosa rasmi kwenye ulingo wa sanaa biashara kama wasanii wengine wakubwa wa Africa mashariki. Jambo ambalo linatarajiwa kuwa la msingi kwani Beka the Boy anavyo vigezo vyote vya kuwa nyota wa muziki anayeweza kuwakilisha nchi ya Kimataifa. Chini hapa nimekusongezea video ya wimbo wake mpya kwa jina nyota, video imeongozwa na kutayarishwa na Kevin Bosco.

 

 

Comments

comments

You may also like ...