Header

Matajiri wa Ufaransa na England wataa Ubingwa wa Ligi

Matajiri wa Jiji la Manchester, Manchester City pamoja na Klabu ya Ufaransa PSG zimetangazwa kuwa Mabingwa wa Ligi kuu kabla ya Ligi kumalizika.

Manchester City walikuwa wa kwanza kutangazwa kuwa Mabingwa wa EPL 2017-2018 baada ya Mpinzani wao Manchester United kupoteza Mchezo wao dhidi ya Washika Mkia wa Ligi Klabu ya West Bromwich Albion kw akufungwa Goli 1-0 na kufanya tofauti ya alama kati yao na Mabingwa Man City kufikia alama 16 huku ikiwa imesalia Michezo 5 ambayo hata United akishinda yote hawezi kufikia alama hizo.

PSG wamenyakua Ubingwa huo baada ya kuwafunga Mabingwa watetezi Monaco kwa Jumla ya Magoli 7-1 na kufanikiwa kuwa kileleni kwa Tofauti ya alama 17 huku ikiwa imesalia Michezo 5 kumalizika kwa Ligi ya nchini humo.

Pep Guardiola anafanikiwa kuipa Man City taji la Ligi kwa mara ya kwanza tangu aanze kuinoa Timu hiyo, huku ukiwa ni Ubingwa wake wa Pili baada ya kusinda Kombe la EFL mwezi uliopita dhidi ya Arsenal.

PSG na Man City zote zilitolewa kwenye Michuano ya UEFA Champions League, PSG kwenye hatua ya Mtoano dhidi ya Real Madrid huku Man City wakitolewa na Liverpool.

Comments

comments

You may also like ...