Header

BEKA THE BOY-NIKO TAYARI KUBURUDISHA AFRICA MASHARIKI!

Beka the Boy akitumbuiza Mashabiki katika Mseto EAST AFRICA

 

Msanii anayetamba kwa kasi kutoka Pwani ya Kenya Beka the Boy, anasema yupo tayari kuiwakilisha Kenya vyema Africa Mashariki kimuziki. Hii ni baada ya kuhojiwa na kituo cha runinga cha Kiss TV kilichoko jijini Nairobi. Beka the Boy ambaye kwasasa anatamba na kibao chake kipya kwa jina Nyota, yupo jijini Nairobi kwa ajili ya media tour ambayo inatarajiwa kumukuza jina lake ilikutambulika zaidi ndani na nje ya mipika ya nchini Kenya.

 

Beka akiwa ndani ya jengo la Kiss media

Beka the Boy ndiye msanii pekee kutoka Pwani ya Kenya kwasasa mwenye management na label ya kwake kwa jina Double B. Beka anakuwa msanii wa kwanza kuto Pwani ya Kenya kufanya muziki kwa kuzingatia miundo misingi ya kisasa, akiwa kwasasa anafanya kazi chini ya mtayarishi wa muziki na mumiliki wa record label ya DreamLand Entertainment Dr. Eddy huku video ya Nyota ikiwa imeongozwa na Director wa video anaeheshimika Kenya Kevin Bosco.

Katika ziara hii pia Beka the Boy aliweza kuitambulisha rasmi video yake ya Nyota kupitia Mseto Mashariki ambayo huwa inaongozwa na kutayarishwa na mtangazaji amabaye anaushawishi mkuu Africa Mshariki si mwengine ila ni Mzazi Willy M Tuva wa kituo cha habari cha Citizen ndani ya Club Tribeka. Kuwepo kwa Willy Mtuva katika kukikuza kipaji cha Beka the Boy, kunapelekea hatua mwafwaka zinazo chukuliwa na timu inayosimamia kazi zake za muziki kwasasa. Kitu ambacho kimemfanya Beka the Boy kujiamini kuwa yupo tayari kuiwakilisha Kenya vyema kimuziki Afrika Mashariki.

 

 

 

 

 

 

 

Comments

comments

You may also like ...