Header

Atletico Madrid yakabidhi mapema Ubingwa wa La Liga kwa Barcelona

Baada ya Klabu ya Atletico Madrid kupoteza Mchezo wa Jana wa Ligi ya Hispania dhidi ya Real Sociedad kwa Magoli 3-0, Vinara wa Ligi hiyo Barcelona wanahitaji alama 3 tu ili waweze kutangazwa Mabingwa wapya wa Ligi Msimu huu 2017-2018.

Atletico ambao wamekuwa Wapinzani wakubwa wa Barca tangu Msimu huu kuanza wakiwa nafasi ya Pili kwa kujikusanyia alama 71 Mpaka sasa katika Michezo 33 huku ikiwa imesalia Michezo 5 tu kumalizika kwa Ligi wamekubali Ubingwa uelekee Catalan baada ya kukubali Kichapo kutoka kwa Real Sociedad.

Kama Barcelona itashinda Mchezo ujao dhidi ya Deportivo La Coruna unaopigwa April 29 basi watakuwa Mabingwa wapya wa Msimu huu kabla ya kukutana na Mahasimu wao Klabu ya Real Madrid kwenye Mchezo wa marudiano wa Ligi.

Mpaka sasa Barcelona ina alama 83 na ikishinda Mchezo ujao wa Ligi itafikisha alama 86 ikiwa imebakiwa na Michezo Minne na kuifanya iwe timu yenye alama nyingi ambazo hakuna Timu inaweza kuifikia hata ikishinda Michezo yote. Mara ya mwisho Barcelona ilishinda Ubingwa wa La Liga Msimu 2015-2016.

Comments

comments

You may also like ...