Header

Snura;- Meneja wangu hausiki kwenye mapenzi yangu.

Msanii wa Muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania, Snura Mushi a.k.a Snuu Sex amesema Meneja wake HK hachangii kitu chochote kwenye mahusiano yake ya kimapenzi.

Akipiga story na Dizzimonline msanii huyu ambae kwasasa anafanya vizuri na kibao chake cha ‘Vumbi la mguu’ amesema meneja wake yupo kwa ajili ya kusimamia kazi zake tu za muziki na sio mahusiano yake ya kimapenzi.

“Labda niseme kitu kimoja ukiona nimefanya kitu chochote kwenye mapenzi au chochote kinachotokea  kwa mpenzi wangu basi fahamu meneja wangu hajachangia kitu chochote hapo ni mimi mwenyewe tu” Amesema Snura.

Aidha Snura ametoa ahadi kwa mashabiki zake kuwa hivi karibuni ataachia Movie ya ‘Vumbi la Mguu’ hivyo waandelee kuwa karibu na msanii huyo.

Comments

comments

You may also like ...