Header

Elycent apandisha Bendera ya hip hop kwa kutamba kama Aslay

Msanii wa muziki wa rap kutoka nchini Kenya, Mwakima Elisha a.k.a Elycent amezungumzia mabadiliko ya biashara ya muziki na ukubwa wa kukubalika kwa muziki wa hip hop na rap tofauti na ilivyokuwa  kipindi cha nyuma.

Akipiga Story na Dizzim Online juu ya mapokezi ya wimbo wake mpya wa ‘Hip Hop Is Back’ , Elycent amethibitisha kuwa muziki wa kuimba ulifanya vizuri kibiashara ambapo amesema kuwa anachokiona ni uwezekano mkubwa wa kila rapa mkali kutengeneza pesa nyingi kwenye muziki wa hip hop kwa sasa.

“Manzeeeee…hip hop is on fire right now na hawa singers they can confess bout that. when I say hip hop is back namaanisha imerudi na ubaya tena kwa ubaya Boss. Vile narogaa na nachora lines na tusiende mbali, lets jump on my new jam ‘Hip Hop Is Back’ can tell that na hiyo hata rappers wa Kenya na East Africa hawabishani”. Amesema  Elycent.

“Nimeachia Song na nashukuru Mungu inajipush bila mimi kutumia nguvu kubwa, so! from there unaweza amini kuwa kwa sasa hivi from hip hop ground tunaweza tengeneza pesa mob ya muziki tofauti na vile ilikuwa kitambo, so kikubwa we need support tu ya mafans”. Ameongeza.

Hata hivyo Elycent anasikika akimtaja Aslay katika wimbo wake huo mpya na alipoulizwa juu ya kutambua soko la muziki la Aslay, aliongeza kuwa moja ya soko la muziki linalokuwa katika mawazo yake pindi anapokuwa akiandaa muziki mzuri kwa mashabiki ni Soko la Tanzania na nchi tofauti zinazotumia na kuelewa lugha ya Kiswahili.

Itazame video mpya ya wimbo wake ‘Hip Hop Is Back’.

 

Comments

comments

You may also like ...