Header

Ezden The Rocker ajichimbia kuandaa Watangazaji Bora, Azingatia kupambana na mapungufu yaliyopo

Mtangazaji kijana kutoka nchini Tanzania, Ezden Jumanne ‘Ezden The Rocker’ ametoa sababu za kuanzisha mpango wake wa kutoa mwanga na mafuzo ya kuandaa watangazaji wenye tija katika vizazi vijavyo vya wanagazaji Bora.

Akipiga Story na Dizzim Online, Ezden amesema kuwa katika ufatiliaji wake wa michipuko ya idadi kubwa ya watangazaji wapya amegundua kuwa sio wote wanaofata taaluma ya uandishi wa habari na utangazaji kwa kuzingatia misingi bali wanaingia katika taaluma hiyo kwa matamanio na kimbilio la umaarufu.

“Nimekuwa mtangazaji na najua kuwa nahitaji kuwa mtangazaji mwenye faida katika jamii yangu lakini kwa sasa waliowengi wanapenda sana aina moja ya sehemu ya taaluma hii lakini wanasahau kuwa wakiwa wengi soko litakosa changamoto na thamani zao zitashuka kutokana na mkumbo wa kutaka aina moja ya vipindi na mfumo wa utangazaji” Amesema Ezden.

Hata hivyo Ezden kwa sasa anajihusisha na uingizaji na unadaa wa sauti za matangazo na mpango wake wa kutoa ushauri na kuandaa kizazi cha vijana watangazaji wenye mwanga katika siku zijazo nao pia anawanoa kwa kuwafundishwa ujuzi na namna ya kandaa matangazo.

Comments

comments

You may also like ...