Header

BASATA kuwapa tuzo za sanaa wanafunzi wa Sekondari

Mkurugenzi Ukuzaji Sanaa na Masoko Basata Vivian Shalua

Baraza la Sanaa Taifa la Tanzania (BASATA) limeandaa tuzo kwa wanafunzi wa shule za sekondari waliofanya vizuri kitaifa katika masomo yao ya Sanaa.

Tuzo hizo zitafanyika tarehe 28/04/2018 katika ukumbi wa BASATA ulioko Ilala Sharif Shamba jijini Dar es Salaam ambapo kwa mujibu wa taarifa rasmi ya Baraza hilo ni kuwa tuzo hizo zitachangia pakubwa katika kujenga wasanii bora na wenye maadili katika kiwanda cha Sanaa siku zijazo.

Tuzo hizo zitahusisha shule 6 za Sekondari ambazo ni Shule ya Sekondari Mbeya, wanafunzi wawili(2), Shule ya Sekondari Dodoma, mwanafunzi mmoja, Edmund Rice Sinon Secondary School iliyoko Arusha, mwanafunzi mmoja ,Shule ya Sekondari Mvuha iliyoko Morogoro, mwanafunzi  mmoja, na Shule ya Sekondari Murugwanza iliyoko Mkoa wa Kagera wanafunzi wawili.

Hata hivyo Baraza hilo limeamini kuwa zoezi hilo la utoaji tuzo litachochea kwa asilimia kubwa wanafunzi kusoma masomo ya Sanaa, kuongeza Ubunifu katika kazi za Sanaa na kuwasaidia katika kuongeza ufaulu wao darasani katika kuzingatia Sanaa kuwa nyenzo katika kumuandaa mtoto kielimu na kimaadili.

Comments

comments

You may also like ...