Header

Ice Boy avundika Kolabo yake na Jose Chameleone

Msanii wa muziki wa kizazi cha rap Tanzania, Ice Boy ametoa sababu na changamoto za kutchelewa kwa kolabo yake na wasanii wa nje ya Tanzania ikiwemo yake na Jose Chameleone.

Akipiga Story na Dizzim Online, Ice amesema kuwa muda wowote anaweza kuachia kolabo alizowashirikisha mastaa wa nje na kuhusu wimbo aliomshirikisha atauachia pale atakapojiridhisha kuliteka soko la Tanzania.

“Mimi Nyimbo ninazo kibao hasa hizi kolabo za mastaa wa East Afrika lakini naamini bado nahitaji kuwafikia mashabiki wengi wa muziki wangu Tanzania ndo nianze kuwaza nje sasa. Ile ya Jose Chameleon ni itatoka tu na ukizingatia yule ni kama Brothe kwangu na ukiachilia hilo naamini nitafanya naye ngoma nyingine” Amesema Ice Boy.

Ice boy anayefanya vizuri na ngoma yake ‘USAWA HUU’ amesema kuwa muda wowote ataachiakolabo yake na mwimbaji Maua Sama itakayokwenda kwa jina ‘Badman’ na kuhusu utayarishaji ameomba chumba cha habari kiisubirie taarifa hizo kama ‘Surprise’.

Comments

comments

You may also like ...