Header

Meek Mill aachiwa huru kutoka Jela, Furaha yatanda Mitaa ya Philadelphia

Staa wa muziki wa rap kutoka Philadelphia, Pennsylvania, Marekani, Robert Rihmeek Williams a.k.a Meek Mill ameachiwa huru juu ya hukumu yake ya kwenda jela Miaka 2-4 iliyotekelezwa na akaanza kuitumikia Mwezi Novemba mwaka jana kutokana na kukiuka masharti ya kuishi kwa kufuata sheria uraiani chini ya uangalizi ‘Probation’.

Mahakama kuu ya jimbo la Philadelphia, Pennsylvania imemuachia huru rapa Meek kupitia hatua ya kisheria ya kupinga hukumu ya awali kutokana na kugundulika kuwa hukumu haikuzingatia haki bali ilitolewa kwa uonevu na chuki za chini zilizokuwepo kati ya Meek na Jaji Genece Brinkley aliyehusika katika hukumu.

Mahakama hiyo imefikia maamuzi ya kufuta kesi ya Meek baada ya siku 60 na taarifa hiyo njema imepokelewa na mastaa kibao marekani ambapo Meek aliutumia ukurasa wake wa Instagram kuwashukuru wote walioshiriki kwa namna yoyote yay eye kuwa huru sasa.

“I’d like to thank God, my family, my friends, my attorneys, my team at Roc Nation including Jay Z, Desiree Perez, my good friend Michael Rubin, my fans, The Pennsylvania Supreme Court and all my public advocates for their love, support and encouragement during this difficult time. While the past five months have been a nightmare, the prayers, visits, calls, letters and rallies have helped me stay positive. To the Philadelphia District Attorney’s office, I’m grateful for your commitment to justice – not only for my case, but for others that have been wrongfully jailed due to police misconduct. Although I’m blessed to have the resources to fight this unjust situation, I understand that many people of color across the country don’t have that luxury and I plan to use my platform to shine a light on those issues. In the meantime, I plan to work closely with my legal team to overturn this unwarranted conviction and look forward to reuniting with my family and resuming my music career.” Aliandika Meek Mill kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Ushindi huo umepatikana baada ya Mwanasheria wa Meek na wato wa karibu kupiga viakali hukumu hiyo na kushirikiana naye bega kwa bega kuhakikisha anakuwa hukuru kwa kuzingatia kuwa haki hazikuzingatiwa na Meek ametangaza kuwa atajihusisha na utetezi wa haki za watu watakao jikuta katika vizingati vya kunyimwa haki zao za kisheria pale zinapohitajika.

Comments

comments

You may also like ...