Header

Mourinho akana kumuuza Mo Salah Chelsea, asema yeye alikubali kumtoa kwa Mkopo tu!

Kocha Mbwatukaji Jose Mourinho amekana kuwa alihusika kumuuza Mshambuliaji wa Chelsea kutoka Misri Mohamed Salah kwenda Roma 2016 huku askisisitiza kuwa yeye alikubali Nyota huyo atolewe kwa Mkopo tu.

Akiwa Kocha wa Chelea, Mourinho alimnunua Salah Mwaka 2014 kutoka Basel ambaye hakufanikiwa kupata nmafasi katika Kikosi cha kwanza kufuatia Majeraha na kutoaminiwa sana na Kocha huyo kabla ya kutolewa kwa Mkopo kwenye Klabu ya Fiorentina Mwaka 2015 kabla ya kujiunga Moja kwa moja na Klabu ya Roma ya nchini Italia.

Salah, 25 amerejea tena England Msimu huu amecheza Michezo na kufunga Magoli 43 akisaidia Liverpool kuwa nafasi ya Tatu kwenye Ligi mpaka sasa huku wakiwa katika nafasi ya Nusu fainali kwenye Michuano ya UEFA.

Baadhi ya Wachambuzi na Mashabiki wa Soka wamekuwa wakimlaumu na kumshangaa Mourinho kwa kitendo cha kutompa nafasi Salah na kuamua kumuuza lakini Kocha huyo amewajibu wakati akihojiwa na kituo cha ESPN.

“Kwa mara ya kwanza nitalizungumzia hili maana kumekuwa na Maneno ambayo yanazungumzwa kuhusu mimi na si sahihi wanasema mimi nilimuuza Salah! ni uongo mimi ndie nilimnunua na nlikubali aende kwa Mkopo” Alisema Mourinho.

“Maamuzi ya kumuuza kupata pesa na kutumia kununua Wachezaji wengine sio langu na hata kama lingekuwa langu kwenye Mpira tunafanya makosa mara nyingi”

Salah anatajwa kuwa Moja ya Washambuliaji bora Duniani kwa sasa huku baadhi ya Wachambuzi wa soka wakisema anastaili kuwa Mchezaji bora wa Dunia kwa sasa huku wengine wakisema ni kati ya Wachezaji watatu bora yaani nyuma ya Ronaldo na Messi.

Comments

comments

You may also like ...