Header

Naibu Spika wa Bunge Dkt. Tulia Ackson abariki Mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018

Kuelekea Mashindano ya Mbeya Tulia Marathon 2018 yatakayofanyika Mkoani Mbeya katika Uwanja wa Sokoine Naibu Spika wa Bunge ambaye ni Muazilishi wa Tulia trust Dkt. Tulia Ackson amezindua rasmi mashindano hayo Siku ya Leo jijini Dar es salaam.

Mashindano hayo ambayo yako chini ya Taasisi ya Tulia trust iliyoanzishwa Mwaka 2015 na Naibu Spika yatafanyika Mei 6 Mwaka huu jijini Mbeya ambapo yatahusishwa washiriki mbalimbali kwa umbali tofauti tofauti.

 

Akizungumza hii leo na Waandishi wa habari wakati wa Uzinduzi rasmi Naibu Spika amesema kuwa lengo lao ni kuhakikisha wanasaidia Jamii kama ilivyo kauli mbiu yao huku pia akiwashukuru Wadhamini na Wadau wote wanaoendelea kuwaunga Mkono.

 

Comments

comments

You may also like ...