Header

‘Hat trick’ ya Messi yaipa Barca Ubingwa wa La Liga bila kupoteza Mchezo wowote

Klabu ya Soka ya Barcelona imetangazwa kuwa Mabingwa wapya wa Ligi kuu nchini Hispania maarufu kama La Liga baada ya kuibuka na Ushindi wa 4-2 dhidi ya Derpotivo La Coruna kwenye Mchezo uliopigwa Siku ya Jana kwenye Uwanja wa Estadio Riazor.

Katika Mchezo huo Nyota wa Barcelona Lionel Messi alifunga Magoli Matatu yaani Hat trick na kuisaidia Barcelona kunyakua Ubingwa Msimu huu 2017/2018 bila kupoteza Mchezo wowote mpaka sasa ukiwa ni Ubingwa wao wa 24 wa La Liga.

Barcelona ilikuwa inahitaji alama 3 tu katika Michezo Minne iliyobaki baada ya Atletico Madrid kupoteza dhoidi ya Real Sociedad Wiki iliyopita kwa Magoli 3-0.

Barcelona itakutana na Wapinzani wao Real Madrid ‘El Classico’ Mei 6 wakati tayari wamenyakua Ubingwa, Mpaka sasa Barca imeshinda Mataji Mawili Ubingwa wa La Liga pamoja na ule wa Copa Del Rey chini ya Kocha Mpya Ernesto Valvede huku pia Nyota Mpya wa Klabu hiyo Phillipe Coutinho akiwa tayari ameanza kuonja Mafanikio ndani ya Barca.

 

Comments

comments

You may also like ...