Header

Jaguar na Prezzo warudisha amani na Upendo

Msanii wa muziki kutoka nchini Kenya, Charles Njagua Kanyi a.k.a Jaguar na msanii mwenzake Jackson Makini a.k.a ‘Prezzo’ wamemaliza tofauti zao za muda mrefu.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Jaguar aliweka picha ya pamoja akiwa na Prezzo na kuthibitisha kuwa wamemaliza tofauti zao na kilichopo ni urafiki wa maisha ya kawaida mpaka kwenye sanaa.
_
“Met up with my colleague and brother CMB @prezzo254
For long, we chose to walk on different paths despite chasing the same dream.
A lot was said over the years, but we have come to the conclusion it is time to rise above our differences and focus on the betterment of our entertainment industry as we prepare ground for those that come after us.” Aliandika Jaguar.

Mapema leo Naye Prezzo aliweka ujumbe wenye uthibitisho kuwa urafiki umerudi kati yake na Jaguar na inaonekana kuwa kuna utayari wa wawili hao kushirikiana pale watakapohitaji kufanya hivyo.

@prezzo254: Kama wengi mnavojua mimi na ndugu yangu @jaguarkenya tulkuwa na friction miaka nenda, miaka rudi ila Mungu alitupatanisha tukaamua kusahau yalio pita na focus kwa ya lio mbele. Iam glad we burried the hatchet now lets put in work my brother…. Bless up#Rapcellency.

Msisitizo wa jaguar katika kumaliza tofauti zao ni kuwa wanania ya kutengeneza mfano mwema kwa wasanii na wote wenye ndoto za kufanikiwa katika maisha yao kwa kujifunza mambo kupitia wao.

Comments

comments

You may also like ...