Header

Miss Eastern Zone 2012, RedButterfly ajitosa rasmi kwenye muziki

Mrembo na Miss Eastern Zone mwaka 2012, Rose Lucas ‘Redbutterfly’ ameingia rasmi kwenye tasnia ya muziki na kutoa sababu zake za kupiga hatua hiyo iliyoambatana na ujio wa wimbo wake mpya kwa jina ‘Nifikishe’.

Akiongea na Dizzim Online, RedButterfly amesema amekuwa katika njia za kufuata ndoto zake kama muimbaji na kikubwa kilichomsukuma kwa sasa kuanza kufanya muziki ni utayari na kukamilika kwa baadhi ya mipango na misingi ya kufanya kazi za muziki.

“kipaji kipo siku nyingi sema nilikuwa sijiweki sana kwenye muziki kwakuwa nilikuwa Busy sana na mambo mengine, Nilikuwa Busy na Shule baadae nikaingia kwenye Mashindano ya ulimbwende. Sasa hivi nimejipanga kuonesha kipaji changu na nijiona mbali kuwakilisha taifa langu kama wanavyofanya akina Vanessa, Diamond Platnumz, AliKiba na wengine” Amesema RedButterFly.

Wimbo wake mpya umetayarishwa na Prodyuza Rigtone ambapo video imeandaliwa, kuongozwa na kukamilishwa na Director

Hata hivyo RedButterfly ameongeza kuwa tayari amejipanga kuachia wimbo mwingine wa pili ndani ya mwezi wa 6 mwaka huu ambao amehaidi kuwa utazingatia viwango na ubora katika uandaaji.

“Mashabiki siwezi kuwaangusha kabisa kwasababu ukiacha hii nimeshaandaa wimbo mwinginemzuri na naamini wataupenda, wimbo huo ambao utakuwa ni wa pili nitauachia mwezi wa Sita mwaka huu” Aliongeza.

Wimbo wa kwanza wa Redbutterfly ‘Nifikishe’.

 

Comments

comments

You may also like ...