Header

Davido atoa zawadi ya wimbo na Gari kwa Mpenzi wake ‘Chioma Avril’

Staa wa muziki kutoka nchini Nigeria, David Adedeji Adeleke ‘Davido’, ameachia video ya wimbo wake mpya kwa jina ‘Assurance’ jina lililoonekana kwenye sherehe za kumbukumbu ya siku ya kuzaliwa kwa mpenzi wake, mrembo Chioma Avril siku ya jana.

Davido aliitumia siku ya jana kuonesha upendo wa dhati katika sherehe zilizoandaliwa kwa ajili ya Chioma Avril aliyekuwa anatimiza umri wa miaka 23 kwa kumpa zawadi ya gari aina ‘Porshe’ na katika eneo la namba za usajili wa gari lilionekana jina la wimbo huo ‘Assurance’.

Wimbo huu Maalum kwa ajili ya Mpenzi wake, Umeingia sokoni chini ya Davido Music Wolrdwide ‘DMW’ kwa utayarishaji wa Prodyuza Speroach Beatz na Video kuongozwa na Director Meji Alabi chini ya kampuni yake ya utayarishaji wa video ‘AJM Film Production’.

Itazame Video ya wimbo huo.

Comments

comments

You may also like ...