Header

Khaligraph Jones awapa nafasi ya kwanza ROSTAM kwenye Album yake

Staa wa muziki wa rap kutoka nchini Kenya, Brian Robert Ouko a.k.a Khaligraph Jones amewashirikisha Umoja wa wasanii wawili kutoka Tanzania, Stamina na Roma Mkatoliki ‘ROSTAM’ katika kolabo ya wimbo wake wa kwanza utakaopatikana katika album yake itakatokwenda kwa jina ‘Testimony 1990’.

Khaligraph Jones

Album hiyo itakuwa ni ya tano kutoka kwa Khaligraph na inatazamiwa kutoka rasmi Mwezi Juni, tarehe 12 mwaka huu, siku ambayo ni tarehe ya kumbukumbu ya kuzaliwa kwake.

ROMA na Stamina ‘ROSTAM’.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Khaligraph aliandika.

“About To drop the 1st Banger from the Testimony 1990 Album Thats Supposed to Launch on June 12th and this Here Am Featuring My Brothers From Tanzania Roma and Stamina *ROSTAM*

Hope y’all Ready…. cc @staminashorwebwenzi @romaa2030

#respecttheogs”.

Post hiyo iliambatana na video ya kionjo kifupi cha video ya wimbo wao unaokwenda kwa jina ‘Now You Know’ ambapo video ya kolabo hiyo imendaliwa na kuongozwa na Enos Olik.

Hata hivyo Khaligraph akiachia album hii ya ‘Testimony 1990’, itakuwa ni ya tano kutoka kwake baada ya Point of No Return ya mwaka 2014, Autograph ya 2014, Eff Off ya 2015 na Best of Khaligraph Jones ya 2017.

Comments

comments

You may also like ...