Header

Lady Jaydee afunga kwa uzuni ukurasa wa Msiba wa Mama yake mzazi

Msanii mkongwe wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Tanzania, Judith Wambura ‘Lady JayDee’ kwa uzuni ameweka picha aliyoitumia kushukuru wote waliomfariji na kushiriki katika Msiba wa mama yake mzazi, Bi. Martha Mbibo uliofanyika Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara.

Lady JayDee ameweka ujumbe huu kwenye ukurasa wake wa Instagram na kubainisha kuwa picha iliyoambatana na ujumbe huo itakuwa ni ya mwisho kutoka kwake kuhusu taarifa za msiba kwakuwa umemalizika kwa mujibu wa taratibu.

“Tumemaliza kuzika salama nashukuru, Maziko yamefanyika kijiji cha Manyamanyama, Wilaya ya Bunda , Mkoa wa Mara|
Na hii ndio picha ya mwisho kwenye page yangu kuhusu msiba, maisha mengine lazima yaendelee|
Picha zilizobakia nita post @ladyjaydeediary @ladyjaydeediarykwaajili ya ndugu jamaa na marafiki kuona kama wakipenda
———————————————————————————————————-
Niwashukuru tena Mzee wangu Chacha Mwita Gachuma 🙏🏽 kwakuwa na mimi siku zote za shida na raha|
Rafiki Anthony Diallo|
Na familia/ Ukoo wa watu wetu kijijini wote waliohudhuria |
Mzee Stephen Wasira hivi nimshukuru?? Kwakuwa yuko kwenye picha tu ila yeye ni family na kila alilofanya ni jukumu lake kama baba angu.
—————————————————————————————————————
Shukrani zingine kwa Nilesh Oil State|
Mh. Elibariki Kingu @ellykinngu |
Kaka angu @professorjaytz |
Octavian Mshiu |
@ivvycarter |
@jembenijembe |
@bertillerm
@cathymagige Asante kwa kuja hadi kijijini kwetu , ur one in a million .
Hayo mengine ya kwako hayanihusu🙈🙈🏃🏽‍♀️🏃🏽‍♀️ ——————————————————————————————————————
Sisi huwa hatuna 40 , kwahiyo msiba umeisha rasmi 🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽🙏🏽
Asanteni na poleni wote mlioguswa |
Msinione kazini mkaanza kuni judge|
#BingwaWaKujihami
#MarthaMbibo
#Mama❤️
#YamekwishaRasmi
#KandaMaalum” Alindika Lady Jaydee.

Bi. Martha Mbibo alifariki tarehe 26, 2018 akiwa nyumbani kwake  baada ya kuugua Saratani kwa muda mrefu.

Comments

comments

You may also like ...