Header

Wema Sepetu; “Afrika sina Timu Kwenye Kombe la Dunia, nitashabikia England tu”

Muigizaji na Mjasiriamali maarufu nchini Wema Abraham Sepetu amesema kuwa kuelekea Kombe la Dunia Mwaka 2018 litakalofanyika nchini Urusi Mwaka huu ataishabikia Timu ya Taifa ya England huku akisisitiza kuwa hana Timu ya kuishabikia Barani Afrika katika zile zilizofuzu Michuano hiyo.

Akizungumza na Dizzimonline wakati wa Uzinduzi rasmi wa Kombe la Dunia kupitia Kampuni ya Star Media Tanzania Limited kupitia Chapa yake ya StarTimes ambao wataonesha Michezo yote 64 kupitia king’amuzi chao kwa Lugha ya Kiswahili, Wema amesema Licha ya kuwa anatamani Timu za Afrika zifanikiwe zaidi kwenye Kombe la Dunia la Mwaka huu lakini hana Timu anayoishangilia zaidi ya England.

“Sijui kwanini zilikuwa hazifanyi vizuri huko nyuma, nadhani ni kujipanga na Maandalizi tu, sina timu ambayo ntashangilia Afrika Timu yangu ni England naipenda England kwa kuwa mimi ni Mshabiki wa Manchester United hivyo ntaipa Supports na natamani ifike mbali zaidi”. Alisema Wema Sepetu

Licha ya England kutofanya Vizuri Wema anaamini Mwaka huu utakua tofauti. Mwanadada huyo anayetamba kwa sasa kwenye Soko la Bidhaa kupitia Product yake ya Lipstic amechagulia kuwa miongoni mwa Mabalozi wa Star times kupitia kombe la Dunia Mwaka huu ambapo Kampuni hiyo itakua na dhamana ya kurusha Mtangazo kwa Lugha ya kiswahili kwa Michezo yote 64.

Comments

comments

You may also like ...