Header

Steven Nyerere na wanauzalendo kwanza wafanikisha kombe la Aweso ‘Aweso Cup’ wilaya ya Pangani

Moja ya mambo makubwa yaliyofanyika wikiendi iliyopita ni tukio kubwa la uhamamishaji vijana kuepuka kupoteza muda wao katika mambo yasiyo ya msingi na kutengeneza mazingira ya kutumia kila fursa iliyopo kwenye mazingira yake ya kila siku kwa lengo la kujitengenezea kipato, kujenga misingi imara ya uchumi wa taifa na kutimiza ndoto za kila kijana lililoongozwa na umoja wa wanauzalendo kwanza katika katika uwanja wa Kumba ulioko wilaya ya pangani katika mkoa wa Tanga.

Umoja wa Wanauzalendo kwanza hao siku ya wakiongozwa na Muigizaji Steven Mengere ‘Steven Nyerere’ kwa ushirikiano na wasanii wa muziki wa kizazi kipya waliowkilishwa na Nuh Mziwanda siku ya Jumamosi walishiriki zoezi hilo sambamba na uzinduzi rasmi wa kombe la Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso ‘Aweso Cup’.

Wachezaji wa Yanga tawi la Pangani

Katika picha ni matukio ya kilichofanyika katika uwanja wa mpira ambapo mashabiki wa klabu ya timu ya mpira wa miguu ya Yanga na mashabiki wa klabu ya mpira ya Simba walipokutana kumenyana mchezo ulioshuhudiwa na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza, Katibu Mtendajiwa Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) Godfrey Mungereza.

Mbunge wa Pangani na Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji, Jumaa Aweso na Mkuu wa Wilaya ya Pangani Bi. Zinabu Issa, Afisa habari wa Simba Haji Manara, Munadishi wa habari Mkongwe Jerry Mulo na wakazi wa Wilaya wenye mapenzi na mpira wa miguu waliungana kuhakikisha kila kitu kinakwenda barabara kwa lengo kuu la kujenga Pangani iliyo imara.

Wageni waalikwa na wachezaji wa timu ya Simba tawi la Pangani(Aliyevaa kofia ni Mbunge wa Pangani Mhe. Jumaa Aweso)

Kilichovutia zaidi na kuzua mazungumzi, kutambiana na furaha kati yao ni matokeo ya mchezo huo ambao ulimalizika kwa dakika tisini za mchezo ambapo Simba waliibuka na ushindi wa magoli mawili kwa moja dhidi ya Yanga.

Wachezaji wa Timu ya Yanga tawi la Pangani wakipasha Misuli kabla ya Mchezo

Shukrani za kutosha ziliwaendea wote walioshiriki na kufanikisha tukio hilo la kimaendeleo ambapo waigizaji wote ambao ni pamoja na Husna Sajenti, Mzee Hashim Kambi, Flora Mvungi, Blandina Chagula ‘Johari’, Kupa, Daudi Michael ‘Duma’, Mayasa Mrisho ‘Maya’, Haji Adam na wengine wengine waliojitoa namna kubwa sana kufanikisha zoezi hilo.

Steven Nyerere na wenzake wakishuhudia Burudani zilizoandaliwa

Wadau na mashabiki wa Mpira wa Miguu waliojitkeza

 

Meza kuu ya wasanii wakiwa wamezungukwa na Mashabiki na wapenzi wa Mpira waliojitokeza

 

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akipokea Cheti cha Ushiriki wa Ufunguzi wa Kombe la Aweso Cup

Mkuu wa Wilaya ya Pangani Mheshimiwa ni Zainabu Issa Meza kuu akiwa na Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza

Naibu Waziri Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Juliana Shonza akiwa meza kuu na mbgunge wa Pangani Mhe. Jumaa Aweso

 

Haji Manara akipeana Mkono na Mkuu wa Wilaya Pangani Mhe. Zinabu Issa

Muigizaji Johari Akishuhudia Mchezo

Comments

comments

You may also like ...