Header

Rayvanny akutana tena na rapa Khaligraph Jones kwenye Remix ya ‘Pochi Nene’

Mastaa wa muziki kutoka nchini Tanzania na Kenya, Msanii Rayvanny na rapa Khaligraph Jones wamekutana kwa mara nyingine kwenye Remix ya wimbo ‘Pochi Nene’ ambao awali uliwahusisha Rayvanny na Mtayarishaji S2kizzy ambaye mbali na kushiriki kama mtayarishaji pia amehusika kuandika na kuimba chorus.

Kupitia ukurasa wa Instagram, Rayvanny aliweka video akiwa studio kwake ‘Surprise Music’ ambapo alikuwa akisikiliza wimbo wake wa Pochi Nene na kutoa taarifa kuwa kuna aliyeshirikishwa kutoka nchini Kenya na ilisikika kuwa ni rapa Khaligraph.

“@rayvanny: Guess Whooooo?????#pochineneRemix Wapo WENGI SAAANA WA KWANZA HUYO anaitwa NANI???? +254 one time 🇰🇪 🔥 Nani unataka kumsikia pia na ITOKE LINI ????#POCHINENE link in My Bio”

Wawili hao walishakutana kwenye kolabo ya wimbo wa Khali uliokwenda kwa jina ‘Chali ya Ghetto’ uliotoka Mwaka jana.

Comments

comments

You may also like ...