Header

Samata A ashangazwa na ‘Aah Kodo’ tofauti na mategemeo yake

Msanii wa muziki na Staa wa ngoma kwa jina ‘Tufyu’, Abdul Ayubu Samata ‘Samata A’ ameshangazwa na mapokezi ya audio na video ya  wimbo wake mpya wa ‘Aah Kodo’ mtaani tofauti na mategemeo yake.

Akipiga Stori na Dizzim Online, Samata A amesema kuwa, nguvu ya mapokeo katika ngoma hiyo iliyotoka sambamba na video iliyoongozwa na Director Joowzey, imeonekana kuchezwa zaidi mitaani tofauti na kwenye vituo vya matangazo vya redio na Runinga.

“Nimeshangazwa sana na mapokeo ya wimbo wangu wa Aah Kodo kwenye mitaa na uswahilini kwa sababu mtaani inafanya poa kuliko hata kwenye media…Nikisema media namaanisha vyombo ambavyo tunaamini vina mchango mkubwa kwenye muziki wetu ili muziki wetu uwafikie mashabiki kwa haraka. Kila mitaa na masherehe ya kitaa utaisikia ngoma zaidi kuliko kwenye tv na redio, sikutegemea hali iwe hivi lakini naamini wanaopenda iwe hivyo ni mashabiki” Amesema Samata A.

Hata hivyo Samata ameachia nyimbo kadhaa zikiwemo ngoma kama vile ‘Totoro’, ‘Wanaboa’ na kolabo yake na Dayna Nyange kwa jina ‘Unanisololo’ ambazo amedai kuwa zimepata mapokeo makubwa ya kuchezwa zaidi kwenye vyombo vya matangazo tofauti na ‘Aah Kodo’.

Video rasmi ya wimbo wa ‘Aah Kodo’.

Comments

comments

You may also like ...